view towards Kilimanjaro from terrace of Kindoroko Hotel


DELUXE
Vifaa Vyote vya Umeme!


VIFAA VYA NGUVU ZA JUA HUFANYAJE KAZI?
  • Africa mashariki ina mazingira muafaka kwa uzalishaji nguvu za jua kwa kuwa jua huangaza kwa kadiri ya masaa 5 kwa siku katika sehemu mbalimbali kwa mwaka. Nishati hii ya jua huweza kutumika katika sehemu zisizokuwa na umeme kutoa nishati ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani kama vile katika taa, redio na Televisheni.

  • Jua linapoangaza kwenye kinasa nishati, huzalisha nguvu kwenye seli maalum ambazo huipa chaji betri.
    Betri huwa ni stoo ambamo nguvu za jua huhifadhiwa na kutumika zinapohitajika.

  • Vyombo vinavyoweza kutumia nguvu hizi za jua ni vile vilivyotengenezwa mahsusi kama taa, redio na televisheni kwani betri huwa na uwezo wa kutoa nguvu za moja kwa moja (Direct Current) za Volti 12. Vyombo vingine vya kutumia umeme vinaweza kutumika pia, lakini gharama yake huwa juu kwa sababu vinahitaji nguvu za Volti 240. kwa hivyo vinahitaji kutumia kibadili (Inverter) kugeuza volti.

  • Pia huhitajika kidhibiti chaji (Charge Controller) kuilinda betri dhidi ya kuzidisha chaji kwenye kipokea miale (Solar Panel) au kuongezeka kwa moto kunakoweza kuchoma vifaa. Bila ya chombo hiki, umri wa betri yako huwa mfupi.

JINSI YA KUCHAGUA NA KUDHIBITI VIFAA HIVI (SOLAR SYSTEM)
  • Ni muhimu kuwa na vifaa vilivyotengezwa sawa sawa ili viweze kufanya kazi vizuri. Ni ryema kununua vifaa vilivyotengenezwa kitaalamu kutoka kwa Sollatek. Kwa kuwa ryombo vyetu vyote hutumia vipuri sawa, Solar Panel katika "Chui Kit" inaweza kuuziwa mtu mwingine unapotaka kununua kifaa kikubwa chenye nguvu nyingi zaidi.

  • Bora kifaa chako (Solar Panel) kimepata mwangaza wa jua kwa masaa sita kuchaji betri, vifaa vinavyoonyeshwa hapa vimeundwa kuweza kukupa masaa manne ya mwangaza kila jioni (isipokuwa kwa starter kit ambayo inahitaji siku mbili kuichaji kabisa betri yako). Majira ya mvua, itakulazimu kupunguza matumizi ya taa na vifaa vingine kutokana na ukosefu wa mwangaza wa kutosha wa jua kuweza kuchaji betri yako kila siku. Ni muhimu kusafisha vifaa vyako mara kwa mara ili vikuhudumie vyema zaidi.

  • Unaweza kutumia vifaa vidogo kama vile redio au Televisheni badala ya taa kwa masaa manne kwa usiku, bora mahitaji ya vyombo vyako yawe sawa na ya taa ambazo hukuziwasha. Redio hutumia nguvu sawa na za balbu moja ilihali Televisheni ndogo ya inchi 14 isiyo ya rangi (Black & White) hutumia nguvu sawa na za balbu mbili.

SOLAR PANELS






The different components of our solar set guarantee an excellent product.
KWA NINI KUCHAGUA VIFAA VYA SOLLATEK?
  • Solar panel ya Watt 14 kwenye "Chui Kit" huja na hakikisho (warranty) kwa miaka sita na Sollatek Charge Controller na taa (bila balbu) ina garantii ya miaka mitano.

  • Vifaa vikubwa huwa na Unisolar Panels zisizovunjika zilizo na garantii dhidi ya hitilafu zozote kwa miaka 20. Taaluma mpya ya Triple Junction Technology katika hizo Unisolar hukupa asilimia 15 zaidi ya nishati katika miezi mitatu ya kwanza ya matumizi, na vyombo vyako havipotezi nguvu hata moto ukizidi. Kinyume na vifaa vya kampuni nyingine ambavyo hupoteza asilimia 20 ya nguvu zake na kuathiri hali ya kuchaji betri. Unisolar Panels pia hufanya vyema siku za mawingu na zina uwezo wa kuhimili vivuli kutokana na kuangukiwa na majani au kinyesi cha ndege ambaryo aghalabu huathiri utendaji kazi wa vifaa aina nyingine.

  • Sunpower 6 Charge controller hutumia kiasi cha milliamp 4 za uwezo wa betri, ambako zile za aina nyingine hutumia mara kumi zaidi, na ina viwango maalum rya kudhibiti volti ambaye hukuhakikishia maisha marefu kwa betri yako.
    Ecolite za watti nane, hutoa mwangaza zaidi kuliko taa ya watti kumi katika soko.Betri ya nguvu za jua ina gerenti ya mwaka mmoja na ukiiona inakufaa zaidi, unaweza kuinunua peke yake kutoka kwa mwuzaji yeyote na bei yake itapunguzwa kutoka kwa vifaa vyote.

  • Wauzaji wote wa vifaa vya Sollatek wana mafundi waliopata mafunzo kutoka kwa Sollatek kukuunganishia ryombo vyako rya nguvu za jua na gharama itategemea mahali na wingi wa vifaa vitakavyohitajika.

ANWANI YETU

DELUXE
S.L.P. 87
MOSHI
TANZANIA

Simu: (+255) 027-2750097
Fax: 027-2750097 /2751149
Mobile: (+255) 0744 269811

Email: deluxe@kicheko.com
dharmjoshi@yahoo.com

<< back to English